LIFE BEFORE WIFI: THE HILARIOUS TALE OF A KENYAN VILLAGE PUPIL
By LERTE MAXWELL
Copyright © 2025 LerteMaxwell Publishers. All rights reserved.
---
“Hii life ya nowadays si mchezo… sisi tulikua tunacheza na matawi tukifurahia kama tuko Dubai!”
Aaah! Life ya shule enzi hizo ilikuwa movie! Na sio ile Netflix movie ya kizungu na helicopter, hapana. Hii ilikuwa ya real, ya mtaa, ya kijijini, ya mti wa mulberry, ya kwa kina Njoro, na ya kuoga kwa mtungi huku ukifukuzwa na mama juu umekaa na shati la shule hadi saa moja usiku.
Ukiamka saa kumi, kwanza unachapa mchele wa jana na chai ya maziwa ya ng'ombe halafu unachomeka kwa barabara na ile kiatu ya bata ya plastic ikilia kwata kwata kila step. Ukifika shule unakuta msee wa prefect ameshika karatasi anasema, “Leo wako kwa list... Otieno, Chepchumba, na wewe Maxwell juu ya kukosa kuleta PTA money.”
1. The Morning Madness - Kunywa chai kama unaenda race ya Olympics
Sasa imagine hii: saa kumi na dakika kumi na tano, bado uko kitandani. Unaskia mama yako:
“Umeamka? Saa hii walimu wako wako kwa parade!”
Wewe unakurupuka, unavaa uniform ya jana yenye ina maploti ya ugali, then unahepa kama unaenda kuokota pesa barabarani. Hakuna brushing, hakuna kufunga shoelace, unapita kwa fence ya neighbor na kushuka kwa shimo lenye tulitengeneza kama shortcut.
Iyo shimo? Ilikuwa passport ya watoto wengi. Ukiipita, ujue umeokoka.
2. Shule yenyewe - Mwalimu ni kama CID
Tukiwa class, mwalimu alikuwa kama polisi wa Flying Squad. Ukihepa homework, anaingia class na kusema:
“Today, I want volunteers… Otieno! Come here!”
Ukisikia jina lako, machozi inakam before you even move. Umesimama hapo mbele na ile punishment ya kuandika “I will always do my homework” mara 200 imeanza kuingia kama tattoo kwa kichwa. Alafu mwalimu akisema, “Enda ukakojoe na urudi,” hiyo ilikuwa trick. Ukirudi, unaambiwa:
“Sasa niko na nguvu mpya ya kukupiga vizuri.” 😂
3. Breaktime – Mabeshte, maandazi, na mchezo ya "kati"
Hii ndiyo part tulikuwa tunangojea. Breaktime ilikuwa world cup ya childhood. Kuna wale walikuwa na pesa – walikuwa na five bob ya maandazi mbili na juice ya tangawizi (ile ya kusababisha tumbo kuimba jioni).
Sisi wengine? Tulikuwa tunaficha mkate kwa socks ama lunch ya boiled maize kwa tissue. Na mchezo?
Cheki hizi:
Kati – na ile raba ilikuwa imechoka hadi inaonyesha strings.
Brikicho – kukimbizana hadi kwa choo.
Bano – ulikuwa na “Kofa”, “Shimo”, na yule msee always anasema “Sikuletangi yangu home.”
Na usisahau ile style ya kusema:
“Usicheze na hii bano yangu, ni original ya Dubai! Ni cousin yangu aliniletea!”
4. Drama ya After School – Homework vs Mbio kwa mto
After school ilikuwa saa ya kuamua. Uende kwa mto kuogelea, uende kucheza kalongolongo, ama uende nyumbani kusaidia kuchota maji. Wengine walikuwa na majukumu serious – kuchunga mbuzi, kufagia boma, ama kusafisha pishi ya ugali ya jana.
Lakini unakumbuka ile homework ya madam Njoki haijafanywa. So unaleta “combined effort” – unakimbilia kwa beshte anajua kusoma, unamuambia:
“Bro, niko na blanko, print yako nipe ni duplicate.”
Na hapo unaandika kwa mwangaza wa moto ya kibiriti hadi jicho inauma.
5. Siku za Baraka – Siku ya kuvalishwa viatu vipya
Ulikuwa unajua uko serious pupil kama ulipata viatu vipya term mpya. Ukingia class na viatu za Bata Ngoma fresh, kila mtu anageuka.
“Uyo ndiye amerudi Nairobi!”
Sisi wengine tunavaa socks kwa chini ya kiatu kuhide ile imechanika mbele. Na ukikanyaga mdomo ya kiatu inatoka kama smile emoji. But you still walk with confidence like minister of education.
6. Creativity ya Kijijini – Toys na brain power ya NASA
Who needs PlayStation when you had a wire car? Ilikuwa masterpiece! Tulikuwa tunatengeneza gari ya waya, gari ya plastiki ya Blueband container, radio ya mawe na kinanda ya kuimba kwa kiberiti.
Msee mmoja alijaribu kutengeneza simu na tin can na string, aliniambia: “Ukizungumza kwa hii, mtu ako kwa choo atasikia.” 😂
Hakuna mtu alitaka kuamini haingewezekana. Maana sisi tuliamini chochote ni possible.
7. Kienyeji Discipline – Slap zenye zilikuwa GPS
Ukikosea home ama shuleni, ulikuwa na chance ya kupata “double deal”. Mwalimu akikuacha, mama yako anakuchapa kwa kusema:
“Nani alikuzalia? Ulikuwa kwa tumbo yangu miezi tisa halafu unaniabisha hivi?!”
Na ile slipper ya Ngoma ilikuwa na GPS – inakufuata hata ukikimbia corner ya nyumba.
8. Village Values – Heshima, Ushirikiano na Kukula kwa pamoja
Kijijini tulikuwa kama familia moja. Hata ukikosea kwa neighbor, mama yao anakuchapa halafu anakuletea nduma kwa dinner.
Mimi niliwahi enda kwa sherehe nikiwa na short ya school, nilikula mpaka nikauliza:
“Hii ni birthday ya nani?”
Nikaambiwa:
“Sio yako lakini chakula ni ya watu wote.”
Ile community love ilikuwa genuine. Leo huwezi pika ugali bila mtu kuuliza kama ni party.
---
Sasa Nini?
Technology imeleta mambo mob, lakini ile roho ya utoto tulikuwa nayo haipatikani kwa TikTok.
Tulicheka bila data, tulicheza bila screens, na tulifurahia maisha bila likes. Na hata kama tulikuwa wachafu, hatukuwa na stress za kudownload homework.
Sisi ndio tulikulia kwa choo ya shimo, kwa chalkboard ya rangi ya kijani, kwa kusikiliza One People Radio kwa redio ya National. Na tulikuwa happy! Very happy!
---
“Ukiona msee anacheka akiona jembe, ujue aliwahi adhibiwa nayo.”
Kwa wote tuliosoma enzi hizo – najua unacheka sasa. Acha tusiwahi sahau enzi hizo, maana humo ndipo tulijifunza kusmile kwa machungu na kucheka kwa shida.
Kwa watoto wa siku hizi – poleni, mmechelewa kuonja tamu ya maisha ya bila password.
---
Copyright © 2025 LerteMaxwell Publishers
Written by LERTE MAXWELL – Proudly from the soil, for the soul.
Comments
Post a Comment